1. Home
  2. Lyrics
  3. Bridget Blue – Ningelijua (Lyrics)
Bridget Blue – Ningelijua (Lyrics)

Bridget Blue – Ningelijua (Lyrics)

2
0
Partager

Bridget Blue – Ningelijua (Lyrics)
Ningelijua ulienipangia
Nisinge lalamika bila kujua
Ningejua vita ulivyonipigania
Nisingeogopa vitisho vyao

Kama ningejua maumivu yangu
Yalikua kisa cha shule ya imani
Ningejua kimya Wako
Ilikua sababu, siyo tharau

Ningejua wakati ulinyamaza
Kumbe ulikua unatenda njia zako
Ningejua milango uliyofunga
Kumbe zilifungwa nisije nikaanguka

Sasa najua — Wewe ni mwaminifu
Sasa najua — rehema zako hazichoki
Sasa najua — ulipanga yote kwa wema
Ee Bwana, Wewe ni wa ajabu

Ningelijua — ningekushukuru mapema
Ningelijua — ningekuinua kwa wimbo
Ningelijua — ningesujudu kwa furaha
Sasa najua — Wewe ni Mwema

Wewe ni Alfa, Wewe ni Omega
Mwanzo na Mwisho, hakuna mwingine
Wewe ni Bwana wa vita vyangu
Uliyeanza ataimaliza

Ni Wewe eeh! Ni Wewe eeh!
Mfalme wa amani, ni WeWe eeh!
Ni Wewe eeh! Ni Wewe eeh!
Uliyeanza ataimaliza!

Ee Bwana, umejua njia zangu
Kabla sijazaliwa, uliniita
Ee Bwana, ulijua mwisho wangu
Hata kabla sijaanza safari

Sasa najua, Wewe ni mwaminifu
Sasa najua, rehema zako hazina mwisho
Sasa najua, kila kilichonitesa
Kilikua darasa la imani yangu

Ee Mungu, umekuwa mwangalifu
Katika kimya chako ulitenda makuu
Na leo nasema, kwa moyo wa shukrani
Ningelijua — ningekusifu mapema

Visites : 2 Aujourd’hui | 2 Totales

Partager

LEAVE YOUR COMMENT

Votre adresse e-mail ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *

Prouvez votre humanité: 9   +   9   =  

error: Droits d'auteur !!!